Tabora Waonja Maji ya Ziwa Viktoria!

Published: April 21, 2020, 9 a.m.

Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kutoka Solwa Mkoani Shinyanga hadi Itumba Tabora umegharimu Shilingi Bilioni 605 na unawanufaisha wakazi milioni moja na laki mbili katika vijiji 102 vya Mikoa ya Shinyanga na Tabora na miji ya Nzega, Igunga, Isikizya na mji wa Tabora.

Mradi huu umejengwa na miundombinu mipana ikiwemo bomba kubwa kutoka Solwa kwenda Itumba Tabora lenye urefu wa Kilomita 280 lna enye kipenyo cha Sq/m 1000 sawa na Mita 1 linalosukuma maji lita milioni 54 kwa siku.

Mradi mzima katika Mkoa wa Tabora una jumla ya matanki 29 huku kubwa zaidi likiwa nje kidogo ya Mji wa Tabora katika eneo la Itumba likiwa na uwezo wa ku- hifadhi maji lita milioni 9.

Hii inamaanisha watakaofikiwa na mradi watanufaika kwa asilimia mia moja.