Nchini Kenya inakadiriwa kuwa mtu mmoja kati ya watu 10 anaugua shida ya akili, Huku mtu mmoja kati ya watu wanne wenye ugonjwa wa akili anahudhuria vituo vya afya.
\nWagonjwa wengi wa akili ujipata wametengwa katika jamii na wanaonekana kama waliolaniwa.
\nJijini Mombasa kumefunguliwa makao na kituo maalumu ya kuwahudumia wagonjwa wa akili cha Women Empowerment for Mental illiness Treatment and Rehabilitation Centre kufunguliwa eneo la Miritini.
\nKituo hicho kwa sasa kina hifadhi zaidi ya wagonjwa akili 65, huku zaidi ya 50 wakiwa wamepona.
\nBY: Athuman Luchi.