Watu Wenye Ulemavu Wanavyotunza Mazingira Mombasa

Published: Feb. 24, 2022, 8:59 a.m.

Kufuati kukithiri kwa mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira duniani,Hapa jijini Mombasa watu wenye ulemavu wamejitosa katika utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira.

\n

Watu hao wenye ulemavu chini ya shirika la 'Tunaweza Women With Disability' wameanzisha mradi wa kutengeneza bidhaa za urembo kama vile bangili,vipuli na shangaa kwa kutumia karatasi aina mbali mbali ambazo urushwa ovyo kwenye majaa ya taka na kisha kuchomwa hivyo kuchafua mazingira.

\n

Mwandishi:Athuman Luchi