Wasichana waendeleza elimu kupitia mchezo wa soka Rabai Part One.

Published: Oct. 10, 2022, 1:12 p.m.

Kijiji cha Jimba, wadi ya Ruruma eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, ni kijiji ambacho kimetegemea sana ukulima kama njia ya kujipatia riziki.

\n

Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kilimo zimepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo basi kupelekea jamii nyingi katika kijiji hicho kuishi katika hali ya chini ya Maisha na kushindwa kujiendeleza kimasomo.

\n

Lakini kuna matumaini ya tatizo hilo kuzikwa katika kaburi la sahau kupitia mchezo upendwao na wengi wa soka.

\n

Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.