Hali ya kiangazi na mabadiliko ya tabia nchi inaendelea kukumba sehemu mbali mbali humu nchini, hivyo basi inasababisha kushuka kwa kiasi kikubwa kwa mazao ya chakula.Hali hii imeathiri mapato na kupanda kwa bei za vyakula.
\nKatika kutafuta suluhu zinazowezekana kukabili hali hii, kikundi cha wanawake wakulima kutoka eneo la Lunga Lunga,walianzisha mradi unaoitwa "agrivoltaics,"yaani kutumia paneli za jua katika ukulima ambao husaidia kukabiliana na hali ya ukame unaozidi kuongezeka.