Wengi hufahamu jina mabuyu yaliyozoeleka kuliwa kwa kumumunya utamu wake ambapo hupikwa kwa kuchanganya na sukari, rangi iwe ya kijani nyekundu au hata njano pamoja na viungo vyengine ambapo badae huuzwa katika paketi kati ya shilingi 5-50
\nLakini je unapomumunya utamu wake unafahamu pale yanapotokaa?.Yanatoka kwa mti wa m'buyu kwa kimombo baobab tree.
\nNi mti mkubwa wa ukanda wa tropiki na matunda yake ndio yanaitwa mabuyu na lile gamba la tunda linaitwa kibuyu na ubuyu ndio hupikwa na kisha tunaomumunya utamu wake.
\nMti wa m'buyu ambao huzalisha mabuyu hustawi sana katika maeneo yenye joto ,yaliyo makavu ya Afrika na una uwezo wa kuhimili makali ya kiangazi.
\nLa zaidi ni kwamba wapo wakulima waliozama katika ukulima wa m'buyu kutokana na manufaa mengi yenye kuendeleza uhai.
\nWakulima hawa wanategemea mibuyu iliyopo mashambani mwao pamoja na ile iliyostawi katika msitu wa Kaya Kauma kaunti ya Kilifi.
\nBy: Mwanaharusi Rashid