Mara nyingi watu wanapougua wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari kutokana na uwepo wa dawa madukani.
\nBila kujua kwamba dawa hizo zinaweza kumletea mtu madhara makubwa kwenye afya yake ikiwemo kufanya magonjwa kuwa sugu.
\nHatua ambayo imepelekea wahudumu wa afya wa nyanjani katika Kijiji cha Ribe eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, kuelimisha wananchi kuhusu taratibu nzuri za utumiaji wa dawa katika Makala yaliyotayarishwa na mhariri wetu Ruth Keah.