Mabadiliko ya tabia nchi yaani climate change, uvuvi haramu,ongezeko la chupa za plastiki baharini na kuharibiwa kwa matumbawe kumetajwa kuwa moja wapo ya mambo yanayoathiri viumbe wa majini na shughuli za uvuvi.
\nLakini ongezeko la joto na kiwango cha maji ya bahari ni miongoni mwa mambo yanayotishia ustawi wa bahari ambayo ni tegemeo kwa Maisha ya binadamu.
\nMhariri wetu Ruth Keah alizuru eneo la Shimoni na kuangazia jinsi jamii ya eneo hilo inavyotunza na kupanda miamba ya matumbawe baharini.