Ulemavu Wangu

Published: April 9, 2022, 7:52 a.m.

Jamii nyingi uhusisha ulemavu na laana pamoja na ushirikina,huku wengine wakihusisha ulemavu huo na  kasoro zinazotokana kwa mzazi haswa wa kike.Kufuatia madai hayo baadhi ya wanajamii uonekana kuwatenga watoto wanaozaliwa na ulemavu.

\n

Ukweli ni kwamba watu wenye ulemavu wako sawa tu kama wengine wasio walemavu.Katika Makala haya \u201cUlemavu Wangu\u201d leo tunaangazia dada watatu waliozaliwa na ulemavu,licha ya baadhi ya watu katika jamii kuwatenga,wazazi wao walijizatiti katika kuwalea na kuwasomesha na kwa sasa wote watatu ni wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wenye ulemavu jijini Mombasa chini ya shirika lao la Tunaweza Women With Disability.

\n

Lucy Chesi pamoja na dadazake wawili wote walizaliwa na ulemavu na cha kufurahisha ni kwamba licha ya kupitia unyanyasaji na kukashifiwa kwa sababu ya maumbile yao,walipuuza kashifa hizo na kujitahidi katika maisha.

\n

Lucy anasimulia stori yake.

\n

By:Trezer Odero