Ukumbatiaji wa Bayoteknolojia kwa usalama wa chakula

Published: Nov. 25, 2021, 5:46 a.m.

Mhogo ni chakula kinachoenziwa na wengi na zao ambalo limewapa wakulima mapato humu nchini.

\n

Chakula chake ni maarufu katika baadhi ya mataifa ya bara la Afrika, Asia na Amerika Kusini.

\n

Kulingana na shirika la utafiti wa kilimo na mifugo humu nchini KALRO, mihogo inapandwa katika hekari laki moja na elfu sabini na mbili nchini ambapo asilimia 60 hupandwa kutoka eneo la Magharibi, Pwani asilimia 30 na eneo la Mashariki likiwa na asilimia 10.

\n

Licha ya kuwa tegemeo kwa wakulima, ukulima huo unakabiliwa na changamoto za maradhi ya aina mbili na kusababisha hasara ya mapato kwa wakulima. Moja wapo ya maradhi hayo ni yale ya cassava brownstreak disease yanayofanya mhogo kuwa rangi ya kahawia na yale ya cassava mosaic ambayo yanaweza kudhibitiwa.

\n

By:Ali Mwalimu