Takwimu zilizowasilishwa kwa kamati ya Seneti ya Afya mwezi Machi na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe zinaonyesha ugonjwa wa mfadhaiko ndio aina ya ugonjwa wa akili unaoenea zaidi nchini.
\nAmina Abdalla ni Mwanzilishi wa kituo cha Women Empowerment for Mental illiness Treatment and Rehabilitation Centre, anasema aliamua kuanzisha makao hayo baada ya kuona hakuna makao ya kuishi ya watu wenye akili punguani wanaorandaranda ovyo mitaani na barabarani.
\nMwandishi: Nuru Mwalimu.