Licha ya Kifungu 81[1c] cha katiba kusisitiza uwakilishi wa usawa na haki kwa watu wenye ulemavu bado wanawake wenye ulemavu waliojitosa kwenye siasa,wanakumbwa na ubaguzi wa kisiasa kutoka kwa wapinzani wao na hata wafuasi wa wapinzani hao.
\nPia kifungu cha katiba cha 27[5] kinaeleza kuwa Mtu hatabaguliwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja dhidi ya mtu mwingine kwa sababu zozote zilizotajwa au kuzingatiwa katika Ibara ya 4.
\nWanasiasa hao wenye ulemavu hukejeliwa na kutengwa katika harakati za kisiasa kufuatia maumbile yao,ubaguzi huo unawaathiri wanasiasa hao wenye ulemavu,hatua inayowafanya wenzao kushindwa kuendeleza azima yao ya kuwania viti vya kisiasa.
\nMwandishi:Nuru Mwalimu