Tamu Tamu ya asali yapotea kwa ukame

Published: Nov. 21, 2021, 11:44 a.m.

Mbali na kuwa mdudu mkali wapo waliozama katika ufugaji wa nyuki kwa ajili ya uzalishaji wa asali kwa matumizi mbalimbali ikiwemo dawa.

\n

Ikumbukwe kuwa si wengi wenye ujasiri na ukakamavu wa kufuga nyuki kutokana na dhana na kasumba kuwa ni wadudu hatari kufuga licha ya kuwa na manufaa tele. 

\n

 Ufugaji wa nyuki hauna mahitaji mengi ikilinganishwa na ufugaji mwengine wowote cha msingi ni mfugaji kuwa na mizinga. 

\n

Kama ukulima na ufugaji wengine wowote ule Nyuki pia hutegemea mvua kwa sababu nyuki hutegemea maua kama chakula na wakati wa mvua ufugaji wa nyuki na uzalishaji asali hushamiri.

\n

By:Mwanaharusi Rashid