Kaunti ya Kilifi katika miaka ya hivi karibuni imetajwa kuwa Moja wapo ya kaunti zinazoongoza Kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimba za mapema nchini.
\nTakwimu kutoka kwa mfumo wa taarifa za afya nchini yaani Kenya Health Information System zikionyesha kuwa jumla ya wasichana 4,909 walio na umri wa kati ya miaka 15-18 walipata mimba katika kipindi Cha mwezi Januari Hadi Agosti Mwaka 2021.
\nNa kama anavyosimulia Ali Mwalimu kwenye makala haya, mashirika mbalimbali kaunti ya Kilifi yamejitokeza kukabiliana na tatizo hilo.