Kutokana na ajali nyingi za barabarani zinazoshuhudiwa humu nchini hasa kwa watu wanaotembea, Serikali iliweka mikakati ya kupunguza ajali hizo kwa kujenga madaraja ya juu ili mwananchi atumie kwa usalama wake mwenyewe.
\nLakini licha ya hatua hiyo ya serikali, bado kuna baadhi ya watu wanaopuuza kutumia daraja hizo,mwishowe huishia kutiwa nguvuni na polisi ama askari wa kaunti kwa kukiuka sheria.
\nMhariri wetu Ruth Keah amefanya mahojiano na baadhi ya watu walioshikwa na kueleza yaliyojiri mikononi mwa maafisa hao wa usalama.