Utunzaji wa mazingira umekua changamoto kubwa sana kote ulimwenguni kwani mabadiliko ya hali ya hewa imeathiri vigezo vingi katika jamii ikiwemo afya, hewa safi, maji safi ya kunywa,chakula na makazi salama.
\n\xa0
\nKufuatia hali hio wanafunzi katika shule ya Salex Transition Academy iliyoko eneo la Mtongwe kaunti ya Mombasa wamejitosa katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi,kwa kutumia mbinu ya kubadilishana chupa za plastiki kwa sodo,miti na vifaa vingine vya masomo.
\n\nFatuma Hamisi mwenye umri wa miaka 13 ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Salex Transition Academy.Yeye ni mwanafunzi wa gredi ya 6 na\xa0 pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira katika shule hiyo.
\nMwandishi:Athuman Luchi
\n