Dawa kali za kulevya kama heroin almaarufu kwa jina unga ni miongoni mwa mihadarati inayojulikana sana Pwani ya Kenya katika miji ya Mombasa, Kwale, Lamu na Kilifi.
\nDawa hizi zimewasababishia watumizi walio vijana, watu wazima waume kwa wanawake hasara kubwa za kiafya, kiuchumi na kijamii.
\nPindi mtu anapoanza ya matumizi ya heroine tabia zake hubadilika pakubwa na sio rahisi kuiacha.
\nUtafiti uliotekelezwa 2016 na profesa Nicole Lee mshirika katika taasisi ya utafiti wa dawa za kulevya, chuo kikuu cha Curtin unaonesha kuwa asilimia 10 ya watu wanategemea pombe na dawa nyingine za kulevya na kwamba kuepuka matumizi huwa ni vigumu baada ya miili yao kuwa tegemezi yani \u201caddicted\u201d na sababu nyingine tofauti.
\nLakini kwa Naima sababu hizo haziikuwa kizuizi kwake kuondoka kwenye uraibu baada ya muda huo wote na sasa ni miaka 7 tangu aanze safari ya kujinasua.
\nKaribu kwenye makala haya ya MUI HUWA MWEMA tukiangazia namna watumizi wa dawa za kulevya wanavyoweza kubadilika na kuwa bora katika jamii jina langu ni Ibrahim Juma Mudibo.
\nBy Ibrahim Juma