Kuwanusuru wanawake na watoto wenye ulemavu waliobakwa Mombasa

Published: March 30, 2022, 7:29 a.m.

Idadi kubwa ya wanawake na watoto wenye ulemavu  wa akili,ulemavu wa kuskia na wale wanaokabiliwa na ulemavu wa kuona wanapitia dhulma mbali mbali ikiwemo ubakaji katika jamii,wengi wa wanaobakwa hutishiwa maisha na husalia kimya wasijue wapi pa kwenda ili kupiga ripoti angalau wapate haki zao za kisheria.

\n

Katika eneo la Kisauni ambapo ninakutana na msichana mwenye umri wa miaka 16 na ambaye ana ulemavu wa akili,pia mtoto huyu ana ujauzito wa miezi 7 alioupata baada ya kubakwa tangu mwezi wa tisa mwaka jana.

\n

By:Nuru Mwalimu