Kukomesha Unyanyapaa na Ubaguzi kwa wanaokabiliwa na tatizo la Afya ya Akili

Published: Oct. 10, 2022, 6:50 a.m.

Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu nchini Kenya asilimia 0.3% ya watu wanaugua ulemavu wa akili jijini Mombasa.

\n

Wengi wa wenye ulemavu wa akili ukumbwa na unyanyapa,msongo wa mawazo na utengwa katika jamii,hivyo wanajipata wakirandaranda mitaani.

\n

Juma Ali ni kijana mwenye umri wa miaka 30, aliyepona matatizo ya akili yaliyomsumbua kwa muda wa miaka 5.

\n

Anasema alianza kurukwa na akili baada ya kumpoteza mchumba wake katika ajali ya barabarani.Anataja kifo hicho kilimfanya kukabwa na msongo wa mawazo na kuanza kutembea uchi na kushambulia watu.

\n

Mwandishi:Athuman Luchi.