Watoto wengi wenye matatizo ya akili upitia unyanyasaji wa kingono,kupachikwa ujauzito na wengi wa wanao bakwa usalia kimya wasijue wapi pa kuripoti kisa hicho,Mariam mwenye umri wa miaka 16 ni kati ya watoto wenye ulemavu wa akili walionajisiwa na kupachikwa mimba.
\nMariam ambalo si jina lake kamili alibakwa na kusalia kimya bila hata kumjulisha mamake.
\nKwa Sasa Mariam analea mtoto mvulana mwenye umri wa miezi mitatu.Anataja kuwa alikuwa ameenda msalaani kujisaidia na huko ndiko alikumbana na jamaa aliyemdhulumu kwa kumbaka.
\nMwandishi:Athuman Luchi