Kifafa ni ugonjwa wa ubongo unaosababisha mtu kupoteza fahamu kwa muda.
\nUgonjwa huu unaweza kumsababishia mtu kufanya vitendo visivyokuwa vya kawaida kama vile kuanguka, kufifitika na hata baadhi ya wagonjwa kutojielewa.
\nKulingana na takwimu kutoka kwa shirika la afya dunia WHO, takriban watu milioni 50 duniani wanaugua maradhi haya, na kuyafanya kuwa miongoni mwa maradhi maarufu zaidi ya ubongo duniani.