Shirika la PELUM Kenya laandaa hafla ya vijana kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana

Published: Aug. 28, 2023, 11:44 a.m.

Vijana zaidi ya 20 walipata fursa ya kujifunza kutoka kikundi cha wazee cha Va-Mweki kutoka eneo la Kivaa, kaunti ya Machakos, nchini Kenya, kuhusu utunzaji wa mazingira kwa kutumia njia ya kitamaduni na uhifadhi wa tamaduni za jamii ya wakamba inayopatikana nchini Kenya.