Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho - Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi

Published: June 18, 2016, 1:17 p.m.

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kiasi kikubwa zinatokana na uharibifu mkubwa wa mazingira, na tayari athari zake zimeanza kujitokeza katika maeneo mbalimbali katika nchi zetu za Afrika Mashariki na Kati. Kipindi chetu cha Mazingira Leo,Dunia Yako inagazia juu ya athari hizo haswa kwa upande wa ongezeko la Joto hali ambayo inatokana na kuharibika kwa tabaka hilo, mionzi mingi zaidi ya jua, huifikia dunia na kurudi angani mara moja kuliko ilivyo kawaida, hali inayosababisha mabadiliko ya tabia nchi yasiotarajiwa, hivyo kusababisha madhara kwa viumbe waishio katika ulimwengu huu.