Kuongezeka kwa kina cha maji ziwa Tanganyika nchini DRC

Published: Aug. 31, 2022, 4:02 p.m.

Kulingana na wataalam, kuongezeka kwa viwango vya maji katika bahari na maziwa yetu, ni miongoni wa ishara za athari zitpokanazo na hali ya mabadiliko ya tabianchi. Kule nchini DRC, miaka mitatu tangu kiwango cha maji katika ziwa Tanganyika kuongezeka kwa karibu mita tano, wafanyabiashara kwenye pwani ya ziwa hilo ambalo linapakana na nchi za Burundi, Tanzania, Zambia na DRC wameendelea kuathirika. Mwenzangu Denise Maheho ametembelea jiji la Kalemie mashariki mwa DRC na kuzungumzo na wafanyabiashara na namna wakabiliana na changamoto ya kuongezeka kwa viwango vya maji vya ziwa Tanganyika.