Kikao cha pili cha kamati ya majadiliano ya kiserikali kuelekea kuundwa kwa mkataba wa uchafuzi wa Plastiki

Published: May 30, 2023, 4:34 p.m.

Ripoti ya hivi punde ya shirika la mazingira la umoja  wa mataifa kuhusu namna dunia inaweza kukomesha uchafuzi wa plastiki imependekeza mabadiliko ya mifumo ili kukabiliana na chanzo cha uchafuzi wa plastiki, mwanzo kwa kupunguza matumizi ya plastiki iliyo na madhara na isiyohitajika na mabadiliko ya masoko kuwezesha kutumia plastiki tena na tena.