Jamii ya Endorois nchini Kenya yataabika kutokana na kupanda kwa kina cha ziwa Bogoria

Published: Oct. 16, 2023, 4:23 p.m.

Kulingana na ripoti ya wataalam, maziwa yanayopatikana eneo la Afrika mashariki yameendelelea kurekodi ongezeko ya kasi ya viwango vya maji, hali inayotajwa kuchangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Nchini Kenya hali hii imeendelea kushuhudiwa kwenye maziwa yanayopatikana katika eneo la bonde la ufa.